Bunge la Libya kuongeza muda wa Utawala

Image caption Mabunge ya Libya

Bunge la Libya linalotambuliwa kimataifa limepiga kura kuongeza muda wake wa utawala uliokuwa ukitarajiwa kumalizika Oktoba mwaka huu.

Lengo kuu ni kuweka nguvu katika juhudi za umoja wa kimataifa pamoja na nchi za Magharibi kupata Serikali yenye nguvu nchini humo.Tokea mwaka uliopita, Libya imekuwa na mabunge mawili hasimu pamoja na serikali mbili zinazoungwa mkono na makundi mawili tofauti ya wanamgambo nchini humo. Msemaji wa bunge linalotambuliwa na Jumuiya za kimataifa amesema wanaunga mkono mazungumzo yanayosimamiwa na umoja wa mataifa yanayofanyika nchini Morocco juma hili.