Mpwa wa rais wa Somalia auawa Mogadishu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia

Mpwa wa rais wa Somali Hassan Sheikh Mohamud ameuawa katika mji mkuu wa Mogadishu.

Ripoti zinaarifu kuwa Liban Osman ambaye alikuwa daktari aliuawa na watu waliokuwa wakiendesha gari katika eneo la Wadajiri lililopo kusini mwa mji.

Waandishi wanasema usalama mjini Mogadishu umeimarishwa katika siku za hivi karibuni ,lakini kundi la wapiganaji wa Alshabaab,linaendelea kufanya mashambulizi ya kiholela likiwalenga wanasiasa.