Waziri mkuu wa Yemen anusurika kifo

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waziri mkuu Khaled Bahah

Waziri mkuu nchini Yemeni Khaled Bahah amenusurika kifo baada ya hoteli aliokuwa akiishi pamoja na baraza lake la mawaziri kushambuliwa katika mji wa Aden.

Milipuko kadhaa ilikumba hoteli ya Qasr siku ya jumanne asubuhi pamoja na makao makuu ya vikosi vya milki za kiarabu vinavyounga mkono serikali pamoja na nyumba moja.

Image caption nyumba ilioshambuliwa

Vyombo vya habari vya UAE vinasema kuwa takriban wanajeshi 15 wa muungano wa Saudia pamoja na wapiganaji walio watiifu kwa serikali waliuawa.

Kulikuwa na ripoti tofauti kuhusu chanzo cha mlipuko huo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hoteli ya Qasr ilioshambuliwa

Msemaji wa serikali nchini Yemen,Rajeh Badi amekiambia chombo cha habari cha AP kwamba roketi zilirushwa katika maeneo matatu kutoka nje ya mji huo.

Hatahivyo,gazeti la eneo hilo Aden al-Ghad lilisema kuwa mlipuko huo ulisababishwa na bomu lililotegwa ndani ya gari.