Rais wa Brazil Dilma matatani

Image caption Rais wa Brazil,Dilma Rousseff

Mahakama nchini Brazil imebaini kuwa Rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff amekiuka sheria za usimamizi wa akaunti ya bajeti ya mwakajana.

Serikali ya nchi hiyo ilishitakiwa kwa tuhuma za kuazima fedha kinyume cha sheria benki kuu kwa lengo la kuziba upungufu wa kibajeti katika serikali kuu

Kambi ya upinzani nchini Brazil imesema kuwa hatua hiyo ya mahakama inawasafishia njia ya kuanza kuchukua hatua za kisheria kumuondoa madarakani Rais wao Rousseff.

Serikali ya Brazil ilishitakiwa kwa tuhuza za kuazima fedha kinyume cha sheria kutoka benki kuu,na hivyo kusababisha upungufu wa fedha za uendeshaji serikali kuu.

Hata hivyo serikali ya Brazil imesema kuwa itakata rufaa kupinga uamuzi huo wa mahakama.