Mapigano Ukingo wa magharibi

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waziri Mkuu wa Israel

Hali ya wasiwasi iliyoikumba Israel na Ukingo wa magharibi imeongezeka baada ya mashambulio kadhaa.

Hali hiyo ya wasiwasi imeelezwa inaweza kusababisha Waziri mkuu wa Israel kukatiza ziara yake nchini Ujerumani.

Katika mashambulio hayo Mpalestina mmoja ameuawa huku wengine watatu wakishikiliwa na polisi, wawili kati yao wakijeruhiwa vibaya kwa risasi.

Raia wanne wa Israel pia wamejeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Kipalestina katika ukingo wa Magharibi na kusini na eneo la kati ya Israel.

Kumezuka mapigano kati ya Waisrael na Wapalestina tangu wiki iliyopita ambapo washambualiaji hao wanadaiwa kuyalenga maeneo ya maalumu ya kumbukumbu za kidini.