Mauaji Australia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi wa Australia wakidhibiti mtuhumiwa

Polisi nchini Australia wamewakamata watu wanne kuhusiana na mauaji ya mfanyakazi mmoja wa polisi.

Mauaji hayo yametokea nje ya makao makuu ya polisi ya South Wales.

Polisi wanasema kuwa mauaji ya Curtis Cheng mjini Sydeny siku ya ijumaa yalihusiana na ugaidi.

Mtu wa umri wa miaka 15 mkurdi wa asili ya Iraq ambaye alimuua mfanyakazi huo naye aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi.