Uingereza yajadili Wahamiaji

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Polisi wa Uingereza akimdhibiti muhamiaji haramu

Suala la uhamiaji limetawala kongamano la chama tawala nchini Uingereza cha conservative.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema serikali yake bado haijaweza kukabiliana na suala la uhamiaji vizuri.

Awali Waziri wa Mambo ya ndani wa nchi hiyo, Theresa May alisema nchi hiyo itatangaza sera mpya kuhusu uhamiaji na utafutaji wa hifadhi kama mbinu ya kupunguza idadi ya wahamiaji.

Alisema mfumo uliopo sasa umepitwa na wakati.