Serikali ya Umoja wa Kitaifa Libya

Haki miliki ya picha
Image caption Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya ametangaza mapendekezo maalumu ya uundwaji wa serikali ya Umoja wa kitaifa nchini humo.

Bernardino Leon ametangaza mapendekezo hayo ikiwa ni matokeo ya mazungumzo ya miezi kadhaa na viongozi wa pande mbili zinazovutana nchini Libya.

Tangazo hilo ni moja ya hatua muhimu katika kutatua mzozo wa pande mbili zinazovutana nchini Libya tangu kuangushwa kwa utawala wa Muamar Gaddaf.

Nchi ya Libya imekuwa katika mgawanyiko wa utawala katika pande mbili yaani utawala wa Kiislam wenye makao makuu yake mjini Tripol na serikali inayotambuliwa kimataifa yenye makao yake mashariki mwa nchi hiyo.

Bunge la pande hizo mbili za utawala unaovutana, linapiga kura kuhusiana na mapendekezo ya Umoja wa Mataifa.

Mapendekezo hayo ni kuwa na baraza la Mawaziri litakalo jumuisha watu 17 na baadhi ya viongozi wa juu serikali wanaotarajiwa kuongoza mwakani.

Mazungumzo hayo yaliyofadhiriwa na umoja wa mataifa yamechukua majuma kadhaa kwa lengo moja la kufanyia marekebisho mapendekezo ya umoja wa mataifa katika kuleta serikali ya umoja wa kimataifa ya Libya

Akizungumza katika mkutano maalumu mjini Skhrat Morocco Bernadino Leon mazingira ya sasa ya kusaka amani ya Libya.

Amesema raia wengi wa Libya wamepoteza maisha yao, watoto wamekuwa wakihangaika,Kwa mjibu wa mashirika ya kimataifa takriban raia milioni 2 nukta 4 wapo katika mazingira ya kuhitaji msaada wa kibinadamu.

Hata hivyo katika mkutano huo mjumbe huyo wa Umoja wa mMtaifa Bernadino leon amependekeza viongozi wa serikali hiyo ya umoja wa kitaifa na kumtaja Fayez al Sarraj kuwa Waziri mkuu na Manaibu wake watatu.