Afrika Kusini yazuia kutawazwa kwa malkia mtoto

Image caption Utamaduni wa Afrika kusini

Mpango wa kundi moja la kikabila nchini Afrika Kusini lenye makao yake mkoani Limpopo wa kumfanya msichana mdogo wa miaka 10 kuwa malkia wa watu hao ni kinyume na sheria, kulingana na tamshi la maafisa wa serikali walionukuliwa katika gazeti la Sowetan mjini Johannesburg.

Hakujakuwa na malkia wa mvua kwa kipndi cha miaka 10 iliopita baada ya kifo cha aliyekuwa malkia.

Kumekuwa na imani kwamba malkia huyo wa mvua ana nguvu maalum,ikiwemo uwezo wa kudhibiti hali ya hewa.