Waafrika waliowahi kushinda tuzo ya Nobel

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Luthuli alikuwa Mwafrika wa kwanza mweusi kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel

Hii hapa ni orodha ya Waafrika waliowahi kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel.

 • 1960 Raia wa Afrika Kusini Albert Luthuli, aliyekuwa kiongozi wa chama cha African National Congress: "Kamati ya Nobel Committee kwa mara ya pili iliteua mshindi kutoka miongoni mwa watu waliokuwa wakihangaishwa na watawala "
 • 1978 Rais wa Misri Anwar al-Sadat alipewa tuzo kwa pamoja na Waziri Mkuu wa Israel Menachem Begin: "Baada ya kufanikisha mkataba wa Amani kati ya mataifa hayo mawili "
 • 1984 Desmond Tutu wa Afrika Kusini, aliyekuwa katibu mkuu wa Baraza la Makanisa ya Afrika Kusini, ambaye sasa ni Askofu Mstaafu wa Cape Town: "Kamati imetambua umuhimu wa jukumu la Desmond Tutu katika kuunganisha wananchi katika kampeni ya kutatua mzozo kuhusu ubaguzi wa rangi Afrika Kusini"
 • 1993 Kiongozi wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini Nelson Mandela, aliyeibuka baadaye kuwa rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini humo, alituzwa kwa pamoja na rais wa mwisho wa enzi ya ubaguzi wa rangi FW de Klerk: "Kwa kazi yao katika kufikisha kikomo kwa amani kwa utawala wa ubaguzi wa langu, na kuweka msingi wa utawala wa demokrasia Afrika Kusini "
 • 2001 Raia wa Ghana Kofi Annan, aliyekuwa katibu mkuu wa UN, alituzwa pamoja na Umoja huo wa Mataifa: "Kwa kazi yao katika kuhakikisha kuwepo kwa ulimwengu wenye mpangilio zaidi na amani "
 • 2004 Mkenya Wangari Maathai, mtetezi wa mazingira na mwanzilishi wa shirika la Green Belt Movement: "Kwa mchango wake kwa maendeleo endelevu, demokrasia na amani "
 • Haki miliki ya picha BBC World Service
  Image caption Wangari Maathai alifariki Septemba 25, 2011
 • 2005 Mmisri Mohamed ElBaradei, mkuu wa shirika la UN kuhusu kawi ya nyuklia, alituzwa pamoja na Shirika la Kimataifa la Kawi ya Atomiki (IAEA): "Kwa juhudi zao katika kuzuia kawi ya nyuklia kutumiwa kwa madhumuni ya kijeshi na kuhakikisha kawi ya nyuklia inatumiwa kwa madhumuni mema na kwa njia salama "
 • 2011 Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf na mwanaharakati wa amani Leymah Gbowee, walituzwa pamoja na Tawakkol Karman kutoka Yemen: "Kwa harakati zao zisizo za kutumia nguvu kutetea usalama wa wanawake na haki kamili za wanawake kushiriki katika kuendeleza amani "
 • 2015 Kundi la National Dialogue Quartet nchini Tunisia, kundi la mashirika ya kijamii: "Kwa mchango wake katika kukuza demokrasia nchini Tunisia baada ya mapinduzi ya Jasmine ya 2011 (yaliyopelekea kung’olewa madarakani kwa Rais Ben Ali."