Watu saba wauawa kwa risasi Burundi

Burundi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Visa vya ufyatulianaji wa risasi Bujumbura vimeongezeka tangu kutekelezwa kwa jaribio la kupindua serikali miezi kadha iliyopita

Watu saba wameuawa katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura kufuatia kinachodaiwa kuwa jaribio la wizi katika benki moja.

Majambazi sita waliuawa na polisi baada ya gari walilotaka kutumia kutoroka kuzuiwa na polisi, polisi wamesema.

Majambazi hao walikuwa wameua afisa mmoja wa polisi awali.

Mwandishi wa BBC mjini humo Prime Ndikumagenge anasema ameona miili mitatu ikiwa katikati mwa barabara na mingine miwili katika kituo cha mafuta kilichoko karibu.

Mwili mwingine ulikuwa mita chache kutoka eneo hilo.