Ghasia:Mkutano wa kisiasa waahirishwa Guinea

Image caption Ghasia mjini Conakry Ghana

Chama cha rais wa Guinea kimeahirisha mkutano wa kisiasa baada ya ghasia kuzuka katika mji mkuu Conakry.

Ghasia hizo zinajiri siku mbili kabla ya uchaguzi wa rais wa taifa hilo.

Waziri mkuu Mohammed Said Fofana ametoa wito kwa raia kutolipiza kisasi ,akiahidi kwamba serikali itawalipa wale ambao mali yao imeharibiwa.

''Hakuna Peuls,Susus wala Manlikes sote ni raia wa Guinea'',alisema akitaja makabila ya taifa hilo ambayo yamegawanyika kisiasa.