Klopp:Kuifunza Liverpool ni changamoto kuu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jurgen Klopp

Mkufunzi mpya wa timu ya Liverpool Jurgen Klopp ameitaja kazi yake mpya katika kilabu hiyo ya Anfield kuwa changamoto kubwa katika kandanda duniani.

Raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 48 aliteuliwa kuchukua mahala pake Brendan Rodgers na hivyobasi kuweka saini kandarasi ya miaka 3 yenye thamani ya pauni milioni 15.

Anachukua kikosi ambacho kiko katika nafasi ya 10 katika jedwali la ligi ya Uingereza kikikiwa na alama 12 kutoka kwa mechi nane.

''Mimi sio mtu wa kukabiliana na mambo rahisi '',Klopp aliambia runinga ya Liverpool .''Hii ndio changamoto kubwa katika soka.Ni kazi ilio na mvuto zaidi katika soka duniani''.