Mkuu wa tume ya uchaguzi ajiuzulu CAR

Image caption Wanajeshi wa umoja wa Afrika

Mkuu wa tume ya uchaguzi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amejiuzulu, na hivyo kuzusha shaka kama uchaguzi wa juma lijalo utafanywa kama ulivyopangwa.

Dieudonne Kombo Yaya,alisema alijiuzulu kwa sababu ya chagizo, kutoka kwa rais na jamii ya kimataifa.

Uchaguzi mkuu umeahirishwa mara mbili, kwa sababu za usalama.

Watu kadha wameuwawa katika ghasia zilizozidi hivi karibuni,huku malaki wakihama makwao.