Mkuu wa tume ya uchaguzi ajiuzulu CAR

Jeruhi apelekwa hospitali katika ghasia za karibuni Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati Haki miliki ya picha car

Mkuu wa tume ya uchaguzi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati amejiuzulu na hivyo kuzusha shaka kama uchaguzi wa juma lijalo utafanywa kama ulivyopangwa.

Dieudonne Kombo Yaya alisema alijiuzulu kwa sababu ya chagizo kutoka kwa rais na jamii ya kimataifa.

Uchaguzi mkuu umeakhirishwa mara mbili kwa sababu za usalama.

Watu kadha wameuwawa katika ghasia zilizozidi hivi za karibuni na malaki wamehama makwao.