Kiongozi wa upinzani azuiliwa nyumbani Moz

Image caption Kiongozi wa upinzani nchini Mozambique Afonso Dhlakama

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Mozambique Afonso Dhlakama aliwekwa katika kizuizi cha nyumbani siku ya ijumaa alipokuwa akirudi kutoka mafichoni baada ya shambulizi la risasi lililowaua wanachama 23 wa ujumbe wake.

Nyumba ya Dhlakama iliopo nje ya Beira ilivamiwa na vikosi vya usalama siku ya ijumaa alfajiri.

Wanachama wake wa usalama walikamatwa huku wakaazi wanaoishi katika eneo hilo wakiagizwa kuondoka huku idadi kubwa ya wanajeshi na maafisa wa polisi wakisalia nje ya nyumba hiyo.

Chama cha Renamokinachoongozwa na Dhlakama kilipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka 16 dhidi ya kile cha Frelimo ambavyo vilimalizika na makubaliano ya amani ya mwaka 1992.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanachama wa chama cha Frelimo

Wasiwasi umezuka tena,katika kipindi cha miaka michache iliopita ,ikiwemo kipindi kilichokaribia uchaguzi wa Octoba mwaka jana ambao Renamo ilishindwa.

Serikali haijatoa sababu ya kukamatwa,ijapokuwa ilisema mwezi uliopita kwamba shambulio hilo la risasi lilianza baada ya maafisa wa usalama wa Dhlakama kuifyatulia risasi texi ya raia.

Lakini Chama cha Renamo kimekana hilo kikisema kuwa Msafara wa Dhlakama ulivamiwa.

''Kizuizi alichowekewa Afonso Dhlakama ni shambulio linalolenga demokrasia na sheria'',mbunge wa chama cha Renamo Ivone Soares alikiambia chombo cha habari cha Reuters.

''Serikali na Frelimo hawawaambii raia wa Mozambique ukweli kwa kuamua kutumia nguvu badala ya mazungumzo''.