Korea Kaskazini yafanya maadhimisho

Haki miliki ya picha AP
Image caption Korea kaskazini yafanya maadhimisho

Gwaride kubwa la kijeshi linafanyika nchini Korea Kaskazini kuadhimisha miaka 70 ya chama tawala cha wafanyikazi.

Gwaride hiyo linafanyika katika mji mkuu wa Pyongyang na kuwashirikisha maelfu ya wanajeshi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Korea kaskazini yafanya maadhimisho

Utawala nchini Korea Kaskazini pia unatarajiwa kutumia sherehe hizo kuonyesha ubabe wao wa zana za kivita.

Mvua kubwa ya usiku kucha imesababisha kuchelewa kwa sherehe hizo kwa saa kadhaa.