Mlipuko wawaua watu 30 Uturuki

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mlipuko waua 30 Uturuki

Milipuko miwili imetokea kwenye mkutano wa hadhara katikati mwa mji mkuu wa Uturuki , Ankara wakati watu walipokuwa wamekusanyika kufanya maandamano ya amani.

Vyombo vya habari vinasema kuwa takriban watu 30 waliuawa.

Picha za televisheni zilionyesha watu waliokuwa na hofu na wengine wakiwa wamelala chini wakiwa wamejaa damu.

Huku duru ya pili ya uchaguzi wa ubunge ikifanyika mwezi ujao , maandanmano hayo yalipangwa na vyama vya wafanyikazi wakitaka kumalizika kwa mashambulizi yanayoendeshwa na serikali dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi.