Boko Haram yaua watu 40 Chad

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Boko Haram yaua watu 40 Chad

Maafisa wa hospitalini wanasema zaidi ya watu 40 wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa kufuatia msururu wa milipuko nchini Chad.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Majeshi ya Chad, ambao wanaisaidia serikali ya Nigeria kupambana na wapiganaji hao

Mashambulio hayo yamelenga soko na kambi ya wakimbizi iliyoko eneo la Baga Sola ufuoni mwa ziwa Chad.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mashambulio hayo yamelenga soko na kambi ya wakimbizi iliyoko eneo la Baga Sola

Kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Boko Haram,limetuhumiwa kwa kutekeleza mashambulizi hayo.

Mashambulizi hayo ya mabomu yalitokea katika mji ulioko Chad karibu na mpaka na Nigeria.

Image caption Kambi ya wakimbizi iliyoko eneo la Baga Sola ufuoni mwa ziwa Chad ililengwa

Raia wengi wa Nigerian walitorokea eneo hilo kujaribu kujinusuru kutoka kwa mashambulio ya wanamgambo hao.

Lakini kundi hilo Boko Haramu limekuwa likiendeleza mashambulio hadi nchi jirani kama Chad, ambao wanaisaidia serikali ya Nigeria kupambana na wapiganaji hao.

Benin, Cameroon, Chad, Niger na Nigeria ziliafikiana kuchangia kikosi cha muungano chenye askari jeshi 8,700 japo kuna madai huenda ukosefu wa ufadhili ndio uliochangia kikosi hicho kutoanza kazi yake.