Mabomu yaua 9 Cameroon

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Milipuko hiyo karibu na Mora imeuwa watu kama 9, na kujeruhi zaidi ya 10.

Wanajeshi wa Cameroon wanasema kuwa kumetokea mashambulio mawili sambamba ya kujitolea mhanga, kaskazini mwa nchi, karibu na mpaka wa Nigeria.

Milipuko hiyo karibu na Mora imeuwa watu kama 9, na kujeruhi zaidi ya 10.

Baadhi ya ripoti zinaeleza kuwa washambuliaji wote wawili walikuwa wanawake.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa Cameroon wanasema kuwa kumetokea mashambulio mawili sambamba ya kujitolea mhanga

Kundi la wapiganaji Waislamu, Boko Haram, limefanya mashambulio ya mara kwa mara katika eneo hilo.