Je nani alaumiwe kwa mabadiliko ya anga ?

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nchi tajiri ndizo zinapaswa kulaumiwa kwa mabadiliko ya anga na athari zake kote duniani.

Nchi tajiri ndizo zinapaswa kulaumiwa kwa mabadiliko ya anga na athari zake kote duniani.

Rais wa Bolivia , Evo Morales amelaumu mataifa hayo yaliyopiga hatua kubwa kiuchumi kwamba ndio wa kulaumiwa kwa hali ya mabadiliko ya anga inayoikumba dunia.

Akizungumza katika mkutano wa kimataifa huko Bolivia uliohudhuriwa na maelfu ya wajumbe kutoka mataifa kote duniani, rais huyo amehoji ni kwanini mataifa ya magharibi yanapenda kukurupuka kuingilia kati mizozo kijeshi na

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Bolivia , Evo Morales amelaumu mataifa hayo yaliyopiga hatua kubwa kiuchumi kwamba ndio wa kulaumiwa kwa hali ya mabadiliko ya anga

kisiasa badala ya kusaidia nchi maskini kukabilina na athari za mabadiliko ya kimazingira ambayo wao ndio wamesababisha.

Ametoa wito mahakama ya kimataifa iundwe kuwawajibisha mataifa yenye uwezo mkubwa kiuchumi yasiochukua hatua za kupunguza athari za mabadiliko ya kimazingira inayotishia dunia kwa sasa.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Kongamano hilo linaendelea sambamba na mkutano mkubwa wa kila mwaka wa benki kuu ya dunia huko Lima Peru.

Maazimio ya mikutano hiyo miwili ni kupata uwiano miongoni mwa mataifa kabla ya kongamano la umoja wa mataifa kuhusu mazingira unaoratibiwa kufanyika Ufaransa mwezi Desemba.