Majeshi ya Syria yakomboa vijiji Idlib

Haki miliki ya picha RIA Novosti
Image caption Majeshi ya Syria yakomboa vijiji Idlib

Wanajeshi wa serikali ya Syria, wakisaidiwa na Hezbollah, inaarifiwa kuwa wamesonga mbele sana dhidi ya wapiganaji, baada ya mashambulio makali ya ndege za Urusi.

Vyanzo vya wanaharakati na serikali, vinasema kuwa jeshi la serikali, limekomboa vijiji viwili katika jimbo la Idlib, kaskazini-magharibi mwa nchi, karibu na barabara kuu inayounganisha miji mikubwa.

Idlib ilikuwa karibu yote imetekwa na ushirika wa wapiganaji, kabla ya Urusi kuingilia kati.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Urusi imefanya mashambulio ya ndege zaidi ya 60 katika saa 24 zilizopita

Urusi inasema imefanya mkutano mwengine, kwa video, na maafisa wa jeshi la Marekani, kujadili njia za kuepuka ajali kati ya ndege za nchi hizo mbili nchini Syria.

Urusi imefanya mashambulio ya ndege zaidi ya 60 katika saa 24 zilizopita.

Wakati huo huo Rais Vladimir Putin wa Urusi, anatarajiwa kukutana na ndugu wa Mfalme wa Abu Dhabi, kujadili vita vya Syria.

Abu Dhabi inaongoza katika Umoja wa Falme za Kiarabu, yaani Imarati.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Urusi na Imarati, zina mchango muhimu nchini Syria.

Urusi na Imarati, zina mchango muhimu nchini Syria.

Urusi imeingilia kati kijeshi, huku ndege zake zikishambulia wapiganaji kumsaidia Rais Rais Assad.

Na Imarati imo katika ushirika, ambao unalenga wapiganaji wa Islamic State, na inaona ni muhimu Rais Assad aondoke madarakani.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Lakini nchi zote mbili, zina masilahi yanayofanana, yaani kupambana na siasa kali za wapiganaji WaIslamu

Lakini nchi zote mbili, zina masilahi yanayofanana, yaani kupambana na siasa kali za wapiganaji WaIslamu.

Mkutano huo unafanywa Sochi, Urusi, ambako mashindano ya magari ya kimataifa, yanafanywa hii leo.