Uturuki yakana mauaji ya Wakurdi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uturuki yakana madai ya kuwashambulia wafuadi wa vyama vya Wakurdi

Waliopanga mhadhara wa amani wa jana, katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara, sasa wanasema, kuwa watu zaidi ya 128 waliuwawa, katika mashambulio mawili sambamba ya mabomu kwenye maandamano hayo.

Serikali bado inasema kuwa watu 95 walikufa, lakini chama cha HDP, kinachopendelewa na wa-Kurd, kinasema kimewatambua maiti wote, isipokuwa wanane tu.

Awali ,Serikali ya Uturuki ilikanusha madai ya vyama vya wa-kurdi kuwa ilihusika katika milipuko hapo jana iliyosababisha vifo vya watu 95.

Msemaji wa waziri mkuu ameshtumu madai hayo , akisema hayana msingi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waziri mkuu wa nchi hiyo Ahmed Davu-Toglu, ametangaza siku 3 za maombolezi.

Uturuki Inasema kuwa watuhumiwa wakuu wa shambulio hilo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu 95 nchini humo ni kundi linalojiita Islamic State na wanamgambo wa ki- Kurdi PKK.

Waliojilipua walilenga mkutano uliokuwa unafanyika wa amani katika mji mkuu wa nchi hiyo Ankara.

Zaidi ya watu wengine 200 wamejuruhiwa katika shambulio hilo baya zaidi kuwahi kufanyika nchini humo.

Waziri mkuu wa nchi hiyo Ahmed Davu-Toglu, ametangaza siku 3 za maombolezi.

Wengi wa walioathiriwa na shambulio hilo ni wanaharakati wanaounga mkono chama cha kiKurd cha HDP, ambacho kimelaumu utawala wa nchi hiyo kwa hali hiyo iliyojiri.

Hata hivyo msemaji wa waziri mkuu ameshtumu madai hayo , amesema watuhumiwa wakuu wa shambulio hilo ni kundi linalojiita Islamic State na wanamgambo wa ki- Kurdi PKK.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Zaidi ya watu wengine 200 wamejuruhiwa katika shambulio hilo baya zaidi kuwahi kufanyika nchini humo.

Picha za televisheni zilionyesha watu waliokuwa na hofu na wengine wakiwa wamelala chini wakiwa wamejaa damu.

Huku duru ya pili ya uchaguzi wa ubunge ikifanyika mwezi ujao , maandanmano hayo yalipangwa na vyama vya wafanyikazi wakitaka kumalizika kwa mashambulizi yanayoendeshwa na serikali dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi.

Kwa upande wao manusura wamezungumzia hisia - mmoja wao Bulent Takdimir amenusurika shambulio hilo lakini marafiki wake wawili wameuawa anaelezea jinsi anavyohofia mustakbali wa badae wa Uturuki:

"Inavyoelekea tutaendelea kushuhudia visa kama hivi, mashambulio zaidi ya mabomu na watu wengine kuawa.....Ndio mambo yanazidi kuwa mabaya ....Hali inaaza kuzorota kuelekea ilipo Syria, Iraq na Libya kwa sasa - Uturuki haiko mbali na hapo."

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Uongozi wa wanamgambo hao PKK, umetoa amri ya kusitisha harakati zao zote za kijeshi

Hata hivyo licha ya tuhuma hizo dhidi ya wanamgambo hao wa Kikurdi waliopigwa marufuku , PKK, uongozi wa wanamgambo hao wametoa amri ya kusitisha harakati zao zote za kijeshi ,hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi November.

Wamesema wanataka kuepukana na vitendo vyovyote ambavyo huenda vikahujumu uchaguzi wa huru na haki.

Makubaliano ya kushitisha mapigano yaliyodumu miaka 2 kati ya PKK na serikali ya uturuki yalivunjika Julai baada ya shambulio la bomu katika mkutano mwengine wakuunga mkono chama cha kisiasa cha wa--Kurdi nchini humo..