Facebook ililipa kodi kidogo kuliko wafanyikazi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Facebook ililipa kodi kidogo kuliko wafanyikazi

Kampuni ya mtandao wa Facebook imelipa kodi ya mapato ya pauni elfu nne pekee yake mwaka wa 2014(£4,327)

Kwa mujibu wa takwimu zilizowekwa wazi na idara inayosimamia maswala ya kodi nchini Uingereza, kampuni hiyo kubwa ilitangaza faida ya zaidi ya dola bilioni $2.9bn.

Kiwango hicho cha kodi ya mapato ilicholipa ni cha chini mno ikilinganishwa na kodi wanayolipa wahudumu na wafanyikazi kwa jumla Uingereza.

Aidha idara inasema kuwa facebook ilisema kuwa ilipata hasara kubwa ya pauni milioni £28.5m kabla ya kutozwa ushuru mwaka wa kibiashara wa 2014.

Kampuni hiyo pia iliwalipa wafanyikazi wake ruzuku ya pauni milioni £35.4m.

Facebook inawafanyikazi 362 nchini Uingereza.

Hii inamaana kuwa kila mmoja wao alipewa takriban pauni £96,000 .

Haki miliki ya picha PA
Image caption Facebook inawafanyikazi 362 nchini Uingereza.

Wadadisi hata hivyo hawaelewi itakuwaje basi kampuni hiyo inalipa kiwango cha chini mno cha kodi ya mapato na wakati huohuo inatoa ruzuku kwa wafanyikazi wake ?

Bila shaka hali hii itachochea mjadala mkali wa iwapo makampuni makubwa yanadanganya kiwango cha faida yanayopata ilikukwepa kulipa kodi ya faida.

Barani ulaya, makampuni ya Google, Amazon, Fiat na Starbucks yanachunguzwa kwa madai ya kukwepa kulipa kodi ya mapato ilihali yanatangaza faida kubwa katika mataifa yao asili kwa maana hii (Marekani)