Auawa kwa kujaribu kumdunga polisi kisu Israeli

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Auawa kwa kujaribu kumdunga polisi kisu Israeli

Maafisa usalama wa Israeli wamempiga risasi na kumuua mwanaume mmoja wakisema alijaribu kumchoma kisu polisi Mashariki mwa Jerusalem leo asubuhi.

Mshambulizi huyo alitambuliwa kuwa wakiarabu.

Polisi huyo ambaye alikua amevaa mavazi ya kujikinga aliepuka shambulizi hilo.

Tukio hilo lilitokea na eneo ambalo kulitokea mashambulizi mwawili hivi majuzi na kusababisha vifo vya watu wawili.

Kumekua na visa vya mashambulizi kadhaa mwezi huu na kuongezeka uhasama kati ya waisrael na Wapalestina ulioanza na ugomvi kuhusu matukio ya watu kunyimwa ruhusa ya kuingia maeneo tukufu kidini kwa jamii hizo mbili.