Uganda kuondoa jeshi lake Sudan Kusini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uganda itaanza kuondoa majeshi yake Sudan Kusini ifikapo mwishoni mwa juma.

Uganda itaanza kuondoa majeshi yake Sudan Kusini ifikapo mwishoni mwa juma.

Kiongozi moja wa kijeshi ameiambia BBC kuwa japo mkataba wa amani uliowekwa sahihi na pande zote hasimu zilipendekeza hilo lifanyike mapema, vikosi vya NRA vitaanza kuondoka karibuni.

Kamanda huyo anasema kuwa hatua hiyo imetokana na haja ya kuundwa kwa jeshi la muungano wa mataifa ya kieneo yaliyopaswa kuchukua pahala pao nje ya mji wa Juba.

Image caption Jeshi hilo la Uganda liliingia Juba yapata miaka miwili iliyopita kwa mwaliko wa rais Salva Kiir.

Jeshi hilo la Uganda liliingia Juba yapata miaka miwili iliyopita kwa mwaliko wa rais Salva Kiir.

Japo wameshurutishwa kuondoka wadadisi wa maswala ya kiusalama na uhusiano wa kimataifa wanakubali kuwa kuwepo kwako viungani mwa jiji hilo kuu la taifa hilo kumesaidia kudhibiti hali ya usalama.