Facebook yatumiwa kuwatafuta mahujaji Mali

Image caption Facebook nchini Mali

Mwanamke mmoja wa Mali amefungua ukurasa wa mtandao wa facebook kwa lengo la kusaidia kupatikana kwa watu 200 kutoka Mali ambao wametoweka baada ya mkasa wa mahujaji nchini Saudia.

Nabou Traore aliiambia BBC kwamba mengi yalikuwa yakifanywa kuwatafuta mahujaji hao waliotoweka.

Watu wamekuwa wakisambaziana picha za ndugu zao katika mitandao ya kijamii kwamba bado hawajawasiliana nao,na vilevile kuwatambua wakiwa hospitalini.

Maafisa wamethibitisha kuwa mahujaji 60 kutoka Mali walifariki wakati wa mkanyagano.

Mamlaka ya Saudia inasema kuwa watu 769 walifariki katika mkanyagano huo,ijapokuwa maafisa kutoka mataifa ya waathiriwa hao wanasema kuwa takwimu za ukweli ni watu 1,480.