EU:Uchaguzi wa Guinea ulikuwa wa haki

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wachunguzi wa muungano wa Ulaya Guinea

Wachunguzi wa muungano wa Ulaya wanasema kuwa uchaguzi wa urais nchini Guinea uliofanyika siku ya jumapili ulikuwa wa haki licha ya matitizo ya kimipango.

Mkuu wa Wachunguzi hao Frank Engels amesema kuwa matatizo hayo ni pamoja na ukosefu wa makaratasi ya kupigia kura na mipangilio isioafikia viwango vilivyohitajika.

Umoja wa bara Afrika umesema kuwa uchaguzi huo ulifanyika kwa njia ya uwazi licha ya matatizo hayo ya kimipango.

Siku ya jumatatu ,viongozi wote wa upinzani walitaka kura hizo kuregelewa mara ya pili kutokana na madai ya udanganyifu.