NEC yaonya dhidi ya kulinda vituo vya kura Tz

Image caption NEC yaonya dhidi ya kulinda vituo vya kura Tz

Agizo la mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, la kuwataka wapiga kura kurudi makwao baada ya kutekeleza wajibu wao wa kikatiba wa kumchagua kiongozi wao limezidi kuibua maswali mengi kutoka kwa viongozi na wawaniaji viti vya kisiasa.

Baadhi ya vyama vimeshikilia kukutu kuwa kamwe havita fuata maagizo hayo kwasababu inakiuka katiba ya taifa inayoruhusu mita mia mbili.

Hata hivyo Mkurugenzi wa uchaguzi katika tume ya uchaguzi ya NEC Kailima R. Kombwey alitoa taarifa ya kuwarai wananchi wasiingilie maswala ya ulinzi wa kura kwani maafisa wa kulinda amani watakuwepo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption NEC imesema kwamba jukumu la kulinda kura litabakia kuwa ya mawakala wa vyama

Aidha NEC imesema kwamba jukumu la kulinda kura litabakia kuwa ya mawakala wa vyama.

Viongozi wa upinzani wamekuwa wakidai kuwa NEC haiaminiki na kwamba itakuwa vigumu vyama hivyo kuwashawishi wafuasi wao kurudi nyumbani baada ya kupiga kura ilihali kuna hofu kuwa huenda kura zao zikaibiwa kwa ajili ya kuifaidi chama tawala.