Je unafahamu kuwa panya wana faida?

Image caption Je unafahamu kuwa panya wanafaida kwa binadamu?

Kwa kawaida panya akionekana machoni pa mwanadamu anauawa ama hata kutegwa na kupewa sumu lakini sio hawa panya wa Sokoine.

Wakaazi wa mkoa wa Morogoro wanafahamu faida ya panya.

Lakini sio hao panya wa mwituni la !

Watafiti katika chuo kikuu cha Sokoine wanafanya utafiti unaohusu panya wa kipekee katika mradi wa Apopo.

Panya hao maalum wanatumika kwa shughuli ya kuchunguza mabomu yaliyofichwa ardhini mbali na ugonjwa wa kifua kikuu TB.

Wanyama hao wanaonasibishwa na uchafu sasa wameiletea Tanzania sifa kwa kuwasaidia watafiti kuondoa mabomu yaliyozikwa ardhini kwa usalama na kupunguza maafa ambayo hutokea watu wanapokanyaga mabomu hao.

Panya hao wa Sokoine wametumika katika mataifa yanayoibuka kutoka kwa vita hapa Afrika na pia duniani.

Image caption Panya hawa kutoka Morogoro wametumika kunusuru jamii katika mataifa ya Angola, Msumbiji na Cambodia.

Panya hawa kutoka Morogoro wametumika kunusuru jamii katika mataifa ya Angola, Msumbiji na Cambodia.

Kazi hii wanaitekeleza kwa urahisi mno kwani wanatumia uwezo wao mkubwa wa kunusa vilipuzi hivyo vilivyozikwa hadi futi moja ndani ya ardhi.

Aidha wanasifika kwa kufanya kazi hiyo kwa kasi na uadilifu kuliko mashine yaliyoundwa mahsusi kwa ajili ya kazi hiyo.

Mwaka uliopita panya hao waliisaidia Msumbiji kutangazwa kuwa taifa lisilokuwa na mabomu yaliyofichwa ardhini.