Playboy kutochapisha picha za uchi wa wanawake

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Playboy

Jarida la Playboy linapanga kuacha kuchapisha picha za wanawake wakiwa uchi wa mnyama.

Wamiliki wa jarida hilo wanasema mtandao umeharibu soko la picha za wanawake wakiwa uchi, na imekuwa vigumu kuuza na kupata faida.

Idadi ya nakala za jarida la Playboy zinazonunuliwa imeshuka kutoka 5.6 milioni miaka ya 1970 hadi 800,000 kwa sasa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Playboy

Hata hivyo, jarida hilo bado litakuwa likichapisha picha za wanawake wakiwa wamekaa kwa njia ya ‘kusisimua hisia’ ingawa hawatakuwa uchi kabisa.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, uamuzi huo ulifikiwa kwenye mkutano uliohudhuriwa na mwanzilishi wa Playboy na mhariri mkuu wa sasa Hugh Hefner, 89.

Maafisa wa jarida hilo wamekiri Playboy imepitwa na wakati na mabadiliko ambayo ilileta wakati wa kuanzishwa kwake 1953.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jarida la Playboy

“Sasa ni rahisi kupata picha za ngono mtandaoni. Picha za jarida sasa zimepitwa na wakati,” afisa mkuu mtendaji wa Playboy Scott Flanders alinukuliwa akisema na jarida hilo.

Tayari tovuti ya Playboy imelazimika kutoweka picha za uchi, ili kuruhusiwa kuhudumu katika mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Twitter.