Ripoti: Thomas Sankara aliuawa kinyama

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Thomas Sankara

Matokeo ya ukaguzi wa kimatibabu uliofanyiwa mabaki ya mwili wa aliyekuwa rais wa Burkina Faso marehemu Thomas Sankara miaka 28 baada ya kuuawa, yanaonyesha kuwa mwili wake ulijaa risasi kulingana na wakili aliyekuwa akiwakilisha familia.

Haya ni kwa mujibu wa ukurasa wa Facebook wa kituo cha habari cha Burkina 24.

Familia yake ilikuwa ikisubiri matokeo ya DNA kuthibitisha kwamba mabaki hayo yalikuwa ya Bw Sankara, wakili Benewende Sankara aliviambia vyombo vya habari nchini humo.

Haki miliki ya picha
Image caption Mariam Sankara mkewe marehemu Thomas Sankara

Bwana Sankara aliuawa katika mazingira ya kutatanisha akiwa na umri wa miaka 37 na kundi la wanajeshi mwezi Octoba mwaka 1987, na alizikwa kwa haraka kufuatia mpainduzi yalioongozwa na mrithi wake Blaise Compaore.