Polisi Israel waweka vituo vya ukaguzi

Image caption Kituo cha ukaguzi nchini Israel

Vikosi vya Israeli vimeanza operesheni kubwa ya maswala ya usalama katika maeneo ya kiarabu ya Jerusalem mashariki,baada ya kuwepo mashambulizi yanayoelezwa kutekelezwa na wapalestina.

Polisi walifunga njia za kuingia wilaya ya Jabal Mukaber, wilaya ambayo wanaume watatu walishutumiwa kuwaua raia watatu wa Israel.

Wanajeshi wa Israel pia wamepeleka mamia ya wanajeshi kusaidia operesheni

baadae,polisi walisema wamemuua kwa risasi Raia wa Palestina aliyemshambulia kwa kisu mwanamke muisraeli katika kituo kikuu cha mabasi mjini Jerusalem.

Mpalestina mmoja ambaye alijaribu kumshambulia kwa kisu Polisi katika lango la Damascus pia aliuawa na polisi.

Tangu kuanza kwa mwezi Oktoba,raia saba wa Israel wameuawa na kadhaa wameruhiwa kwa kushambuliwa kwa risasi na kuchomwa kisu,mamlaka za Israel zimeeleza.

Kwa mujibu wa Wizara ya afya ya Palestina,Takriban wapalestina 30 wameuawa,wakiwemo waliotekeleza mashambulizi,na mamia wamejeruhiwa.