Wanawake waandamana Uganda

Image caption Wanawake waandamana nchini Uganda

Kundi la wanawake nchini Uganda wanaopinga kuvuliwa nguo kwa mwenzao wakati alipokuwa akikamatwa na maafisa wa polisi, limefanya maandamano na kujaribu kuelekea bungeni ili kuwasilisha hoja yao dhidi ya ukatili wa maafisa wa polisi.

Hatua hiyo inajiri baada ya mwanamke mmoja kutoka chama cha Upinzani cha Forum for Democratic Change kinachoongozwa na Kizza Besigye kuvuliwa nguo na maafisa wa polisi alipokuwa akikamatwa wikendi iliopita.

Image caption Waandamana Uganda

Hatahivyo waandamanaji hao walizuiliwa kuendeleza maandamano hayo na kusukumwa hadi katika afisi zao na maafisa wa polisi.

Kulikuwa na jaribio la kuwakamata baadhi yao lakini walikataa.