Daraja laanguka na kuwaua 3 Afrika Kusini

Haki miliki ya picha
Image caption Johannesburg

Watu watatu sasa wamethibitishwa kufariki baada ya daraja la mda kuangukia barabara kuu ya magari mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya jumatano.

Watu wengine 19 walijeruhiwa katika kisa hicho ,kulingana na shirika la huduma za dharura nchini humo.

Meya wa Johannesburg amesema kuwa iwapo uchunguzi wao utabaini kwamba kuanguka kwa daraja hilo kunatokana na uzembe, wale waliohusika watawajibishwa kulingana na mwandishi wa BBC Pumza Filhani mjini humo.

Kampuni ya ujenzi nchini Afrika Kusini Murray & Robert imeanzisha uchunguzi wake.