El Nino: Wenyeji wakaidi onyo la kuhama TZ

Image caption Baadhi ya makazi ya mabondeni,jijini Dar es Salaam

Serikali ya Tanzania kwa muda mrefu sasa imekuwa ikifanya jitihada za kuwahamisha watu wanaoishi mabondeni, maeneo ambayo husababisha majanga kwa wananchi hao wakati wa mvua, vikiwemo vifo na kuharibika kwa makazi yake. Hata hivyo baada ya msimu wa mvua kuisha wakazi hao hurejea katika maeneo hayo yenye hatari.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania imetangaza kuwa huenda kukawa na mvua za El Nino hali ambayo ni hatari kwa wakazi hao iwapo mvua hizo zitawakuta katika maeneo ambayo hawataki kuondoka pamoja na kuambiwa waondoke.

Eneo la jangwani Jangwani lililoko katikati ya jiji la Dar es salaam ,limekuwa likiathirika sana pale inapo nyesha mvua kubwa lakini wakazi wa eneo hili wamekuwa wakihamishwa mara kwa mara na kupelekwa sehemu salama

wakatiwa mafuriko lakini baada ya muda wananchi hawa hurejea na kuendeleza maisha yao eneo hili hili.

Image caption Jangwani,katikati ya jiji la Dar es Salaam

Mwandishi wetu Esther Namuhisa aliweza kutembelea eneo hilo na kupata majibu tofauti tofauti kutoka kwa wakazi hao;

Francis John ambaye ni mkazi wa Bondeni, anasema hali ngumu ya maisha ndio iliyosababisha yeye kuishi katika eneo hilo,"kipato changu nikikiangalia hakikidhi mimi kukaa juu, hivyo ikabidi nikae bondeni,maeneo ya juu chumba

elfu 60 na kipato changu elfu 10 na hapo nina familia ya kuitunza ambayo inatakiwa ile na kusoma".

Francis aliongezea kuwa viwanja walivyopewa na serikali inamuwia vigumu yeye kuhamia huko kwani huku bondeni ana nyumba tayari na kule anapewa kiwanja tu na hema ambalo limechakaa!

Bi Asha pia ni mkazi wa bonde la jangwani,yeye anasema eneo walilopewa na serikali lijulikanalo kwa jina la mabwepande, halifai hata kidogo kwa kuwa ni mbali na mji na hali ni ngumu huko.

Kutokana na hilo amekata tamaa na anaisubiri tu hiyo mvua ya El-nino ije.

Hajali ikiwa wataishia kukaa barabarani na ikiisha watarudi huko katika maeneo yao kama kawaida.

Hana kazi,kazi yake ni kuokota makopo alafu ayauze ili apate kipato cha kuwalipia ada watoto wake.

Aidha anasema kuwa kazi za aina hiyo mabwepande hazipo na eneo hilo ni karibu na mjini ,Soko kubwa la Kariakoo na hospitali kubwa ya Muhimbili.

Wakati Hamisi Juma yeye anasema wamezoea hali yao,wamezaliwa hapo na wana watoto na wajukuu hivyo ni ngumu kwao kuhama labda kama wakiandaliwa miundo mbinu mizuri.

Image caption Ofisi za mabasi ya mwendo kasi yaliyopo Jangwani

Hata hivyo hivi karibuni,ofisi za kituo cha mabasi ya mwendo kasi kimejengwa katika eneo hilo.

Ujenzi huo umewafanya wahoji kama eneo hilo halifai sasa inakuaje serikali imeweza kujenga ofisi zake za gharama katika eneo hilo wakati wao wanaambiwa wahame.

Lakini cha kushangaza eneo hili pia lina ofisi za serikali ya mtaa ambapo niliweza kuzungumza na mwenyekiti wa eneo hilo.

Yeye anadai kuwa wanafanya jitihada wakishirikiana na msaada wa benki kuu ya dunia kusafisha mto wa msimbazi kwa kina cha mita tano kwenda chini huku wakiwa wamejiandaa na mahema ili kuhakikisha kuwa kuna usalama endapo el nino itakapotokea.

Josephine Mwankyusa ni mshauri wa mazingira na sayansi ya jamii katika kitengo cha miundo mbinu upande wa mabasi ya mwendo kasi,anatofautiana na mwenyekiti wa mtaa huo kwa kusema kuwa mradi huo upo kwa ajili ya

kuimarisha mbinu ya ofisi za mabasi ya mwendo kasi ambacho kiwanja chake kilipimwa na kiko mwanzo hivyo bado wakazi hawa wataathirika na hawatakuwa salama hata kidogo.

Eneo la mwabepande ambalo ni km 27 kutoka eneo la jangwani ,eneo ambalo wahanga wa mafuriko katika maeneo ya bondeni waliweza kupewa hifadhi.Baadhi ya wakazi hawa wanasema eneo hili ni zuri bali hali ya kimaisha ni

ngumu sana na vijana wengi wameshindwa kukaa huko,wazee waliobaki wengi wanategemea kuletewa chakula kutoka kwa watoto wao wanaoishi mjini.

Image caption Mabwepande,mji mpya wa wahanga wa mafuriko

Eneo hilo ambalo kwa sasa serikali imeweza kuweka kuweka huduma muhimu za kijamii kama hospital,shule ya msingi na kituo cha polisi lakini bado msaada waliopewa ambao ulikuwa ni kiwanja na mifuko 100 ya cement wengi

wao hawakuweza kufanikiwa kufanikiwa kujenga,bali wachache waliweza kuuza nusu mifuko ya cement na mingine kujengea lakini bado ilikua ngumu kwa wengi kufanikiwa.