Lori laanguka na kuziba barabara muhimu Nairobi

Ajali
Image caption Barabara ya Uhuru Highway hutumiwa kuingia jiji la Nairobi ukitokea upande wa Westlands

Msongamano mkubwa wa magari umeshuhudiwa katika moja ya barabara kuu za kuingia jiji la Nairobi baada ya lori kuanguka na kufuziba upande mmoja wa barabara.

Wengi wa wakazi waliokuwa wakijiandaa kwenda kazini kutumia barabara hiyo ya Uhuru Highway karibu wamelazimika kutumia muda mwingi kufika jijini.

Ajali hiyo ilitokea usiku mita chache baada ya kupita mzunguko wa barabara wa Museum Hill ukielekea Nairobi.

Image caption Lori hilo lilikuwa limebeba mahindi

Magari yanayotaka kuingia jijini yanaelekezwa kutumia barabara ya Kijabe Street, mwandishi wa BBC Bashkas Jugsoday anasema.

Eneo hilo liko karibu na chuo kikuu cha Nairobi.

Image caption Foleni ndefu ya magari imeshuhudiwa katika barabara hiyo

Hakuna ripoti zozote za majeruhi.

Barabara hiyo hutumiwa na watu wanaotoka maeneo ya magharibi mwa jiji na pia magharibi mwa nchi kama vile Naivasha na Nakuru, Eldoret na Kisumu.