Visa viwili vipya vya Ebola vyaripotiwa Guinea

Ebola Haki miliki ya picha
Image caption Ugonjwa wa Ebola umetatiza sana Guinea, Liberia na Sierra Leone mwaka huu

Visa viwili vipya vya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola vimeripotiwa nchini Guinea na kufikisha kikomo muda wa wiki mbili ambao nchi hiyo ilikuwa imekaa bila visa vipya.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kisa kimoja kimethibitishwa katika mji mkuu Conakry na kingine kilomita 70 kusini mashariki katika mji wa Forecariah.

Taifa hutangazwa kuwa huru kutoka kwa virusi vya Ebola likimaliza siku 42 bila kuripoti maambukizi mapya.

Msemaji wa WHO Margaret Harris ameambia kikao cha wanahabari mjini Geneva kwamba “kwenye barabara yenye kupanda na kushuka ambayo tumekuwa tukiizungumzia … tena tumepata matuta kadha,” shirika la habari la Reuters limeripoti.

"Bila shaka hatukutana haya lakini tulitarajia. Guinea haikuwa imefika katika kiwango ambacho tungeanza kuangalia siku 42 (kwa matumaini).”