Uchaguzi wa ubunge waanza Misri

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uchaguzi wa ubunge umesubiriwa kwa muda mrefu nchini Misri.

Shughuli za upigaji kura kuwachagua wabunge zinaanza rasmi leo Jumapili Misri na katika balozo zote za nchi hiyo .

Huu ndio mkondo wa kwanza wa uchaguzi uliocheleweshwa kwa muda mrefu ya kuwachagua wawakilishi wa ubunge.

Wengi wa wagombeaji ni waungwaji mkono wa rais wa zamani na kamanda mkuu wa jeshi, Abdul Fattah al-Sisi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kundi kubwa zaidi la kiislamu la The Muslim Brotherhood -- halikubaliwi kugombea katika uchaguzi huo.

Kundi kubwa zaidi la kiislamu la The Muslim Brotherhood -- halikubaliwi kugombea katika uchaguzi huo.

Kilishinda uchaguzi uliopita wa ubunge miaka mitatu iliyopita.

Hata hivyo vuguvugu hilo lilipigwa marufuku baada ya jeshi kutwaa utawala mnamo mwaka wa 2013.

Haki miliki ya picha
Image caption Uchaguzi wa ubunge umesubiriwa kwa muda mrefu nchini Misri.

Kuna mikondo miwili ya upigaji kura huku matokeo rasmi yakitarajiwa kutangazwa mapema mwezi Disemba.

Uchaguzi wa ubunge umesubiriwa kwa muda mrefu nchini Misri.