India: Watu 2 ndani kubaka mtoto wa miaka 2

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hasira imetanda New Delhi baada ya mtoto wa miaka 2 kubakwa India

Polisi mjini Delhi, India wamewakamata vijana wawili, wanaotuhumiwa kwa ubakaji wa mtoto wa miaka mwili.

Kisa hicho cha ubakaji ni mojawapo wa visa vinavyoendelea mjini humo na kueneza mshtuko mkubwa duniani.

Vijana hao walio na umri wa miaka 17 walitiwa nguvuni baada ya polisi kuwahoji wenyeji wa kijiji kulikotokea tukio hilo la ubakaji.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hasira imetokana na serikali kushindwa kutunga sheria mpya itakayowalinda wanawake na watoto wa kike India

Mkuu wa mawaziri mjini Delhi Arvind Kejriwal ameshtumu serikali kuu ya India kwa kushindwa kuweka sera za kukabiliana na dhulma dhidi ya watoto.

Kumetibuka hasira miongoni mwa wenyeji na haswa wanawake baada ya tukio lingine ambapo kitoto cha miaka miwili kilibakwa na kutupwa kwenye bustani huku akivuja damu.

Wakati huohuo,wanaume wengine 5 wametiwa mbaroni kwa tuhuma za ubakaji wa mtoto mwenye umri wa miaka 5 pekee.

Tukio hilo la pili katika mji mkuu wa India New Delhi lilitokea katika maeneo ya mashariki mwa Delhi.

Haki miliki ya picha ap
Image caption Mji mkuu wa Delhi umeshuhudia matukio 2000 ya ubakaji katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Watoto hao walidanganywa na pipi wakaingia katika nyumba ya jirani yao kabla ya kubakwa.

Kwa sasa watoto hao wanapokea matibabu maalum na wanaendelea kupata nafuu kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika.

Matukio hayo yameibua hasira miongoni mwa wenyeji na hofu miongoni mwa wanawake ambao wana watoto wa kike.

Mji mkuu wa Delhi umeshuhudia matukio 2000 ya ubakaji katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.