Mshambuliaji auawa Israel

Image caption Askari wakilinda usalama katika kituo cha Basi,Israel

Raia mmoja wa Israel ameuawa katika mapambano ya kurushiana risasi na kuchomana visu yaliyozuka katika kituo cha Basi kusini mwa mji wa Beersheva.

Hata hivyo katika mapambano hayo watu wengine kumi walijeruhiwa wane kati yao wakiwa ni Polisi. Mtu aliyetekeleza shambulio hilo anadhaniwa kuwa ni raia wa Palestina ambaye alipigwa risasi na Polisi na kufariki. Inadaiwa kuwa mshambuliaji huyo alifika kituoni hapo akiwa amejihami kwa Bunduki na visu,ambapo alifanikiwa kufyatua risasi. Majeruhi mwinmgine ni raia wa Eritrea ambaye alipigwa risasi na Polisi ambaye alidhani kuwa huyo alikuwa ni mshambuliaji wa pili.

Zaidi ya 50 wamekufa hadi sasa ndani ya wiki tatu kutokana na machafuko nchini humo.