Kimbunga Koppu, chaikumba Ufilipino

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kimbunga Koppu, chaikumba Ufilipino

Kimbunga kikali kiitwacho, Koppu kimeikumba Ufilipino, na kuingia kwa kishindo, hadi katika kisiwa kikuu cha Luzon, huku upepo ukienda kwa kasi ya kilomita 200 kwa saa.

Siku tatu ya mafuriko, upepo mkali na maporomoko ya ardhi, yanatarajiwa huku kimbunga hicho kikiingia taratibu katika taifa hilo la kisiwani, na kufanya kiwango cha maji ya mvua kupanda na kufikia kimo cha mita moja.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kimbunga hicho kimesababisha upepo mkali wa kasi ya mita 200

Mwaandishi wa BBC anasema kuwa utabiri unaonesha kuwa hali mbaya ya hewa itasababisha mvua kunyesha kwa siku kadhaa mfululizo katika eneo hilo.

Usafiri wa ndege umesitishwa, barabara zimefungwa na maelfu ya watu wanaoishi maeneo ya pwani, wakihamishiwa maeneo salama.

Afisa wa shirika la UNICEF Lotta Sylvanda, yuko katika mji mkuu, Manila na anasema kuwa hali ni mbaya mno

Akihutubia taifa kwa njia ya runinga siku ya Ijumaa, rais wa nchi hiyo Benigno Aquino, alitoa wito akiwaomba watu kujiandaa ilikupunguza maafa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kimbunga Haiyan, kilichotokea nchini humo, mwaka 2013

Amefanya hivyo kwa mara ya kwanza tangu janga la kimbunga kikali kiitwacho Haiyan, kilichotokea nchini humo, mwaka 2013.

Zaidi ya watu elfu 5 walifariki katika janga hilo.