Israeli inawasaka waliomuua raia wa Eritrea

Image caption Israeli inawasaka waliomuua raia wa Eritrea

Serikali ya Israeli inajiandaa kuwapa polisi nguvu zaidi ili kukabiliana na wimbi la mashambulio ya visu kutoka kwa wapalestina.

Hatua hiyo inafuatia kuongezeka kwa visa hivyo mwishoni mwa juma.

Wakati huo huo maafisa wa usalama nchini humo wameanza juhudi za kuwasaka watu waliomuua mwanaume mmoja kutoka Eritrea akiwa amelala chini baada ya kupigwa risasi na mlinzi mmoja akidhaniwa kuwa mshambulizi.

Image caption Raia huyo wa Eritrea alipigwa risasi na walinzi waliodhani kuwa alikuwa mshambuliaji wa pili.

Raia huyo wa Eritrea alipigwa risasi na walinzi waliodhani kuwa alikuwa mshambuliaji wa pili.

Video inaonesha kuwa bwana huyo raia wa Eritrea alivamiwa na kupigwa na umati wa watu waliojawa na hasira akiwa amelala chini akivuja damu.

Hakuna aliyemsaidia kunusuru maisha yake .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Israeli wamethibitisha kuwa mshambuliaji katika kituo cha mabasi cha Be'er Sheva alikuwa ni raia wa Israeli kutoka kwa jamii ya wa -bedouini

Maafisa wa polisi nchini Israeli wamethibitisha kuwa mshambuliaji katika kituo cha mabasi cha Be'er Sheva alikuwa ni raia wa Israeli kutoka kwa jamii ya wa -bedouini.

Zaidi ya 50 wamekufa hadi sasa ndani ya wiki tatu kutokana na machafuko nchini humo.