Uingereza yateua balozi mpya Kenya

Image caption Nic Hailey - balozi mpya wa Uingereza nchini Kenya

Bwana Nic Hailey ametangazwa kuwa balozi mpya wa Uingereza nchini Kenya.

Balozi Hailey atachukua nafasi iliyoachwa wazi na kuondoka kwa mtangulizi wake daktari Christian Turner ambaye kipindi chake cha kuhudumu mjini Nairobi kimekamilika.

''Ninafurahia sana kuteuliwa kuwa balozi wa Uingereza wakati huu ambao uhusiano baina yetu na Kenya umechukua mkondo mpya kwa manufaa ya mataifa yote mawili.''

'Ninatazamia kuwasili Kenya'alisema balozi Hailey.

Bwana Hailey atachukua hatamu rasmi mwezi Desemba.

Hailey ambaye amekuwa akihudumu kama mkurugenzi wa afisi ya jumuia ya madola barani Afrika tangu mwaka wa 2013 aliwahi kuwa balozi wa Uingereza nchini Afghanistan, Marekani, Ufaransa na Ujerumani.