Maandamano na milipuko yatikisa Congo Brazzaville

Haki miliki ya picha
Image caption Milipuko imesikika katika mji mkuu wa Congo, Brazzaville, kufuatia maandamano makubwa yaliyoitishwa kupinga rais Sassou Nguesso kuwania muhula wa tatu.

Milipuko imesikika katika mji mkuu wa Congo, Brazzaville, kufuatia maandamano makubwa yaliyoitishwa na vyama vya upinzani kupinga hatua ya rais aliyeko madarakani Denis Sassou Nguesso kutaka kubadilisha katiba ilikumruhusu kuwania muhula wa tatu.

Vyama vya upinzani viliitisha maandamano hayo na inasemekana kuwa wanajaribu kuingia katikati mwa jiji hilo la Brazzaville.

Serikali ilikuwa imepiga marufuku maandamano yeyote kabla ya kura ya maoni itakayoamua iwapo katiba ya taifa itabadilishwa au la.

Mwandishi aliyeko huko amesemakuwa mji huo umezingirwa na maafisa wa usalama.

Haki miliki ya picha Voice of Congo
Image caption Aidha huduma za simu pia zimesitishwa na kufikia sasa watu hawawezi kutuma au kupokea ujumbe mfupi.

Hakuna magari mabarabarani walashughuli za kibiashara za raia zimesimamishwa.

Mawasiliano pia yamekatizwa huku mtandao wa Intanet ukizimwa ilikuzuia mawasiliano.

Aidha huduma za simu pia zimesitishwa na kufikia sasa watu hawawezi kutuma au kupokea ujumbe mfupi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wafuasi wa Sassou Nguesso waliandamana hapo jana mjini Brazzaville

Shirika la redio la Radio France Internationalpia limezimwa.

Sassou Nguesso ambaye anaumri wa miaka 72 ameiongoza taifa hilo kwa zaidi ya miaka 32 katika awamu mbili.

katiba ya nchi hiyo inapendekeza mtu atakayewania urais wa taifa hilo asiwe na umri unaozidi miaka 70.

Vilevile rais hastahili kusalia madarakani kwa zaidi ya mihula miwili.