FIFA kuendelea mbele na uchaguzi wa urais

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption FIFA itaendelea na uchaguzi mwakani

Kamati kuu ya FIFA imeamua kuwa uchaguzi wa urais kumrithi Sepp Blatter utaendelea mbele mwezi Februari mwakani kama ulivyokuwa umepangwa hapo mbele.

Kamati hiyo ilikuwa inakutana kwa mara ya kwanza tangu kupigwa marufuku kwa rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter na rais wa shirikisho la soka barani ulaya Michel Platini kwa tuhuma za kushiriki ufisadi.

Maafisa hao wawili wamekanusha madai hayo yaliyotolewa na kamati ya uadilifu na nidhamu ya FIFA.

Shirikisho hilo pia limethibitisha kuwa litaendelea mbele na kikao chake maalum wakati huohguo.

Uchaguzi huo utamteua kiongozi mpya wa FIFA.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais anayeondoka madarakani Blatter, amekuwa uongozini tangu mwaka wa 1988

Rais anayeondoka madarakani Blatter, amekuwa uongozini tangu mwaka wa 1988.

Mapendekezo mengine yaliyopitishwa ni kuwa shirikisho hilo litakuwa wazi zaidi kwa nia ya kupambana na ufisadi na ulaji rushwa miongoni mwa maafisa wake wakuu.

Aidha uwazi huo unatoa fursa kwa majina ya maafisa wanaochunguzwa kutajwa hadharani.

Vilevile Kikao hicho kilipendekeza kuwa rais atakayekiongoza asizidi umri wa miaka 74.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kauli hii ya kamati kuu ya FIFA inaelekea kuathiri vibaya uwaniaji urais wa Michel Platini ambaye anatumikia marufuku ya siku 90 kwa madai ya ufisadi.

Pia kamati maalum ya uendelevu na mabadiliko ya FIFA imependekeza kuwa rais atakayeteuliwa asizidishe miaka 12 akiliongoza shirikisho hilo linalosimamia soka kote duniani.

Kauli hii ya kamati kuu ya FIFA inaelekea kuathiri vibaya uwaniaji urais wa Michel Platini ambaye anatumikia marufuku ya siku 90 kwa madai ya ufisadi.

Licha ya kuwakilisha karatasi zake za kuomba kura mapema mwezi huu kamati kuu ya FIF imepuuzilia mbali kwani tayari amepigwa marufuku kushiriki vikao vyake mbali na kuwa hawezi kuendesha kampeni yake.

Image caption Mwanamfalme Ali bin al-Hussein wa Jordan alishindwa na Blatter katika uchaguzi uliotangulia

FIFA imesema itamruhusu kushiriki uchaguzi huo iwapo tu marufuku yake itaisha kabla ya siku ya uchaguzi.

Mwengine anayetarajiwa kuwania kiti hicho ni Shaikh Salman bin Ebrahim Al Khalifa wa Bahrain ,Mchezaji wa zamani wa Trinidad and Tobago David Nakhid mbali na mwanamfalme Ali bin al-Hussein wa Jordan aliyeshindwa na Blatter katika uchaguzi uliotangulia.