Mikutano ya Pegida yafanyika Ujerumani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Makundi ya wanaounga mkono Pegida

Kumekuwa na mikutano ya hadhara nchini Ujerumani ya kupinga na kuunga mkono maadhimisho ya mwaka wa kwanza tangu kuanzishwa muungano wa kupinga wahamiaji kuingia nchini humo ujulikanao kama Pegida.

Polisi wanasema zaidi ya wanachama 20,000 wa Pegida walikusanyika katika mji wa Dresden, ambao ndilo chimbuko la vuguvugu hilo.

Wengine walibeba mabango yenye michoro ya mwamake Mwislamu aliyevalia Burka chini ya Msalaba mkubwa wa Kikristo.

Mkutano mwingine wa watu wanaounga mkono wakimbizi uliwavutia zaidi ya watu 7,000.