Hatimaye wahamiaji waingia Slovenia

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maelfu ya wahamiaji wakiwa mpakani mwa Slovenia na Croatia

Slovenia imesema kuwa imewaruhusu karibu wakimbizi na wahamiaji wote waliokuwa wamekwama katika mpaka wake na Croatia kuingia nchini mwake.

Watu wanaokisiwa kuwa 5,000, wengi wao wakiwa wakimbizi kutoka Syria, walikwama nje eneo lenye unyevu, baridi na kwenye matope mnamo Jumatatu huku mataifa ya Balkan yakiendelea kulaumiana mnamo Jumatatu juu ya kubadilisha msimamo juu ya idadi ya watu walioahidi kupea hifadhi.

Mashirika ya kutoa misaada yameonya kuwa hali itazidi kuwa mbaya zaidi kwa sababu maelfu ya watu wangali wanajaribu kuingia Ulaya Kaskazini huku msongamano ukizidi kuongezeka kwenye vivukio kwenye mipaka.