Sudan K: Uganda inaondoa majeshi yake

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Sudan K: Uganda inaondoa majeshi yake

Sudan Kusini inasema kuwa majeshi ya Uganda yaliyoko Jonglei yameanza kuondoka nchini humo.

Msemaji wa serikali ya Sudan Kusini, Michael Makuei, amesema kuwa kikosi hicho kilichoko katika jimbo la Jonglei kimeondoka tayari na kinaelekea katika mji mkuu wa Juba ambapo wataungana na vikosi vilivyoko huko.

Kuondoka kwa majeshi hayo ya Uganda ni mojawepo ya vipengee vilivyo kubaliwa na kuwekwa sahihi na pande zote hasimu katika mazungumzo ya pamoja ya amani huko Ethiopia.

Msemaji huyo amesema kuwa japo kuondoka kwao kulikusudiwa kuanza mapema, shughuli nzima imechukua muda zaidi kutokana na idadi kubwa ya vifaa vya kijeshi vilivokuwa vimetumwa huko.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Sudan Kusini inasema kuwa majeshi ya Uganda yaliyoko Jonglei yameanza kuondoka nchini humo

Hata hivyo, haijajulikana athari za wao kuondoka katika sehemu hizo itakuwa nini kwani walipaswa kuondoka na mahala pao kuchukuliwa na jeshi la pamoja ambalo hata kufikia leo halijaundwa.

Kumekuwa na mapigano ya mara kwa mara baina ya jeshi la serikali na waasi licha ya kuwekwa sahihi mkataba wa amani mwezi Agosti.