Kenyatta aipuuzilia mbali mahakama ya ICC

Image caption Kenyatta aipuzilia mbali mahakama ya ICC

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amepuzilia mbali onyo la jaji wa mahakama ya ICC Chile Eboe-Osuji ya kuwataka wakenya wakome kuijadili kesi inayoendelea kusikizwa dhidi ya Naibu Rais wa Kenya William Ruto na mwandishi wa habari Joshua Sang.

Jaji Eboe alionya wanasiasa wanaoitukana mahakama hiyo hususan katika mikutano ya hadhara ya maombi ambayo imetia fora nchini Kenya.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jaji Eboe alionya wanasiasa wanaoitukana mahakama hiyo hususan katika mikutano ya hadhara ya maombi ambayo imetia fora nchini Kenya.

Akilihutubia taifa katika hafla ya kuadhimisha sikukuu ya mashujaa, Rais Kenyatta amesema

''hata wale wanaotusukumie hii mambo ya icc kila siku mambo ni ICC wawachane na sisi wawache sisi tuendeleee kujenga na kuunganisha wakenya wenzetu.''

Image caption Rais Kenyatta mwenyewe alikuwa anakabiliwa na kesi kama hiyo huko ICC lakini ikatupiliwa mbali

''Na sisi wakenya tuendelee kuomba jaji fulani hawezi kutuambia ati sisi hatuna nguvu ya kuomba ... sisi tunaamini mungu, Na sisi tunauhuru wa kuomba, Na tutaendelea na maombi kwa sababu tunajua maombi faida yake ni nini'."

Uhuru alisema akiashiria onyo la Jaji Chile Eboe-Osuji anayesikiza kesi dhidi ya Ruto na Sang.

Kenyatta alisema kuwa mikutano ya maombi ya kumuombea naibu wake itaendelea.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Naibu rais wa Kenya William Ruto na muandishi habari Joshua arap Sang wakihutubia wanahabari

Naibu wake William Ruto na muandishi habari Joshua arap Sang wanakabiliwa na tuhuma za kuchochea mapigano yaliyosabisha vifo vya watu 1,300 huku wengine laki sita wakihamishwa makwao punde baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007 kutangazwa nchini Kenya.''

Jaji